Confirmation kwenye teknolojia ya blockchain ni uthibitisho kwamba muamala (transaction) fulani umeongezwa kwenye mnyororo wa block (blockchain) na umepokelewa na kuthibitishwa na node nyingi kwenye mtandao. Kila confirmation inaonyesha kuwa muamala wako ni halali na hauwezi kubadilishwa kwa urahisi. Mfano hai: Unapotuma Bitcoin kwa mtu, muamala huo kwanza huingia kwenye mempool (mahali pa kusubiri). Wachimbaji (miners) huuchukua na kuuongeza kwenye block mpya. Mara block hiyo inapoongezwa kwenye blockchain na kuthibitishwa na nodes wengine, hiyo ndiyo confirmation ya kwanza. Kila block inayofuata na kujengwa juu ya hiyo huongeza confirmation moja zaidi. Kawaida, kwa muamala wa Bitcoin, confirmations 6 huchukuliwa kuwa salama kabisa kwa miamala mikubwa. Kwa miamala midogo kama ununuzi wa kahawa, hata confirmation 1 inaweza kutosha. Faida ya confirmation ni kuhakikisha hakuna mtu anaweza kutumia tena Bitcoin ile ile mara mbili (double spending). Pia, inasaidia kuweka usalama na uaminifu kwenye mtandao wa blockchain. Kwa hivyo, confirmation ni kipengele muhimu sana katika kuhakikisha uhalali, usalama, na ufanisi wa miamala ya kidijitali kwenye teknolojia ya blockchain. image